Historia ya Gadaffi (BBC) na mitandao mingine
Kanali Muammar Gaddafi ni kiongozi aliyekaa madarakani kwa muda mrefu zaidi barani Afrika na katika nchi za Kiarabu.
Ameongoza Libya tangu alipompindua Mfalme Idris I, katika mapinduzi yasiyo ya kumwaga damu, wakati huo akiwa na umri wa miaka 27.
Maarufu kwa nguo anazopenda kuvaa, na walinzi wa kike wenye kubeba silaha, kiongozi huyo wa Libya pia anadhaniwa kuwa na mbinu nzuri za kisiasa, kwa kuweza kuirejesha Libya kutokana na kutengwa kidiplomasia duniani.
Baada ya miongo miwili ya kutengwa katika jamii ya kimataifa, mwaka 2003, Tripoli ilikiri kuwa walifanya shambulio la Lockerbie kwa kuiangamiza kwa mabomu ndege ya Pam Am na hapo Umoja wa Mataifa ukaondoa vikwazo dhidi ya Libya.
Baada ya miezi kadhaa, serikali ya Kanali Gaddafi ilisitisha mipango yake ya kuunda silaha za maangamizi na hii ikarejesha ushirikiano na nchi za magharibi.
Hapo ndipo mabadiliko halisi yalionekana kwa kuwa nchi hizo za magharibi zilibadili mtazamo wao na kuacha kumtenga Gaddafi na kushirikiana naye hata kama alikuwa hatabiriki.
Ni mtu wa kipekee katika kauli zake, mienendo yake, tabia zake na mikakati yake, kwa mujibu wa Saas Djebbar mtaalam wa siasa za Libya.
'Lakini ni mwanasiasa mashuhuri; hakuna shaka lolote kuhusu hilo. Ni mwanasiasa anayeweza kuhimili misukosuko ya kisiasa kwa hali ya juu sana.'
Asili ya Mabedui
Muammar Gaddafi alizaliwa jangwani karibu na Sirte mwaka 1942.
Gaddafi alipanga njama ya kupindua utawala wa kifalme alipokuwa mwanafunzi wa kijeshi na aliwahi kupata mafunzo zaidi akiwa Uingereza kabla ya kurejea nyumbani Libya, mji wa Benghazi, na kupanga mapinduzi ya tarehe 1 Septemba mwaka wa 1969.
Ghaddafi alianza kujenga itikadi zake za kisiasa mwaka 1970 na kuziandika katika kitabu chake cha kijani kibichi.
Alikitumia kitabu chake kuanzisha mfumo wa kisiasa iliyojumuisha kanuni za kiislamu na mfumo uliyo tofauti na siasa za ujamaa au ubepari.
MAMBO KUMI (10) YALIYOMO KWENYE GREEN BOOK
1. “Women, like men, are human beings. This is an incontestable truth… Women are different from men in form because they are females, just as all females in the kingdom of plants and animals differ from the male of their species… According to gynecologists women, unlike men, menstruate each month… Since men cannot be impregnated they do not experience the ailments that women do. She breastfeeds for nearly two years.”
2. “There are inevitable cycles of social history: the yellow race’s domination of the world, when it came from Asia, and the white race’s attempts at colonizing extensive areas of all continents of the world. Now, it is the turn of the black race to prevail in the world.”
3. “While it is democratically not permissible for an individual to own any information or publishing medium, all individuals have a natural right to self-expression by any means, even if such means were insane and meant to prove a person’s insanity.”
4. “Mandatory education is a coercive education that suppresses freedom. To impose specific teaching materials is a dictatorial act.”
5. “If a community of people wears white on a mournful occasion and another dresses in black, then one community would like white and dislike black and the other would like black and dislike white. Moreover, this attitude leaves a physical effect on the cells as well as on the genes in the body.”
6. “Sporting clubs which constitute the traditional sports institutions in the world today are rapacious social instruments. The grandstands of public athletic fields are actually constructed to obstruct access to the fields.”
7. “Placing a child in a day nursery is coercive and tyrannical and a violation of the child’s free and natural disposition.”
8. “Labour in return for wages is virtually the same as enslaving a human being. In a socialist society no person may own a private means of transportation for the purpose of renting to others, because this represents controlling the needs of others.”
9. “The democratic system is a cohesive structure whose foundation stones are firmly laid one above the other, the Basic People’s Conferences, the People’s Conferences, and the People’s Committees, which finally come together when the General People’s Conference convenes. There is absolutely no conception of democratic society other than this.”
10. “No representation of the people—representation is a falsehood. The mere existence of parliaments underlies the absence of the people, for democracy can only exist with the presence of the people and not in the presence of representatives of the people.”
Mwaka1977 aliasisi mfumo ujulikanao kama 'Jamahiriya' au 'Taifa la Umma' ambapo raia ndio wanaoendesha uongozi wa nchi yao kupitia 'kamati za umma'.
Mfumo huo wa Gaddafi umevuka mipaka na hauhusishi mambo ya siasa tu, bali pia mambo mengine.
Akiwa safarini ng'ambo, huwa anakaa kwenye kambi iliyojengwa na hema yake ya kifahari ya Kibeduwi akiwa amefuatana na walinzi wanawake ambao, inasemekana, huwa hawapotezi umakini kazini kama walinzi wanaume.
Hema hiyo pia hutumiwa kuwalaki wageni wa Libya na Kanali Gaddafi huendesha mikutano na mahojiano yake humo humo akipepea usinga au tawi la mitende.
Upekepeke wa Gaddafi
Benjamin Barber, mtaalam wa kisiasa wa kujitegemea, kutoka Marekani amewahi kukutana na Gaddafi mara kadhaa hivi karibuni na kuzungumza naye kuhusu mustakabali wa Libya.
Bw Barber alisema kuwa Muammar Gaddafi anajihisi kuwa msomi aliyebobea.
Muammar Gaddafi na Tony Blair waliwahi kuandaa mkutano wa viongozi kutoka nchi mbalimbali tarehe 29 Mei 2007 kwenye hema hiyo ya Kibedui.
"Utashangazwa kuwa ingawaje ni dikteta, ni mwanafalasafa na mwenye kutafakari jambo kabla ya kuzungumza," aliiambia BBC.
"Namchukulia sana kama mtu kutoka kabila la Waberber na mtu ambaye aliibuka kutoka tamaduni za watu wa jangwani, kutoka kwenye mchanga na kwa namna fulani kuna tofauti kubwa na uongozi wa kisasa, na kwa namna fulani hilo limemfanay awe mstahamilivu na mwenye msimamo."
Kanali Gaddafi amejitahidi kwa muda mrefu kutoa ushawishi wake nyumbani na ng'ambo.
Awali alituma jeshi lake nchini Chad ambapo wanajeshi walidhibiti ukanda wa Aozou, kaskazini mwa nchi hiyo, mwaka 1973.
Katika miaka ya 80 aliandaa mafunzo kwa makundi ya waasi kutoka Afrika Magharibi yaliyojumuisha wale wa Tuareg ambao ni Waberber.
Hivi karibuni aliongoza jitihada za kuwapatanisha waasi wa Tuareg kutoka nchi za Niger na Mali.
Kutengwa na jamii ya kimataifa
Jumuiya ya wanadiplomasia kuitenga Libya kulitokana na Kanali Muammar Gaddafi kuunga mkono makundi yeneye silaha, ikiwemo Irish Republican Army na Palestine Liberation Organisation.
Rais wa zamani wa Marekani Ronald Reagan alimwita Gaddafi 'mad dog' yaani 'mbwa kichaa' na Marekani ililipiza kisasi dhidi ya Libya kwa madai ya kuhusika na mashambulio ya anga barani Ulaya kwa kuvamia miji ya Tripoli na Benghazi mwaka 1986.
Ilisemekana kuwa Kanali Gaddafi alitikiswa na mashambulio ya mabomu hayo ambapo mtoto wake wa kike wa kufikia aliuawa.
Aliposhindwa katika jitihada zake za kuzipatanisha nchi za Uarabuni katika miaka ya 90, Kanali Gaddafi alielekeza nguvu zake barani Afrika na kupendekeza 'Muungano wa Nchi' za bara la Afrika.
Alianza kuvaa mavazi yake binafsi, sare za michezo zilizo na ngao za bara la Afrika au picha za viongozi kutoka bara hilo.
Wakati wa mabadiliko katika karne ya 20, huku Libya ikiwa inapata tabu kutokana na vikwazo dhidi ya nchi hiyo, alianza kurekebisha hali nchini mwake.
Mwaka wa 2003, mabadiliko yakaanza kuonekana na baada ya miaka mitano mkataba wa kulipa fidia kwa waathirika wa Lockerbire uliafikiwa na hii ikarejesha uhusiano kati ya Washington na Libya.
'Hakutakuwa na vita tena, mashambulio, na vitendo vya ugaidi' Kanali Gaddafi alisema alipokuwa akiiherehekea miaka 39 aliyokaa madarakani.
Changamoto za ndani
Kiongozi huyo wa Libya hujiona kama kiongozi wa kidini wa taifa hilo, akihakikisha kwa kile anachosema ni demokrasia.
Lakini katika hali halisi, wakosoaji wanasema Kanali Gaddafi amefanikiwa kudhibiti nchi hiyo.
Wanaompinga wamekandamizwa kikatili na vyombo vya habari vinabaki katika udhibiti mkubwa wa serikali.
Libya ina sheria ambazo haziwaruhusi watu kukusanyika katika misingi ya kisiasa zinazopinga mapinduzi ya Kanali Gaddafi.
Walibya wengi wana wasiwasi juu ya mabadiliko yanayotokea na kuhisi kuwa hawapati manufaa kutoka rasilmali ya Libya, waangalizi wanasema kwani huduma za serikali ni duni pamoja na ubadhirifu mkubwa wa mali.
' Wanajihadhari sana katika mapambano hayo kwa kuwa hawataki mabadiliko yatakayolegeza nguvu za umma,' alisema Saad Djebbar
'Lakini wakati huo huo, Walibya wanafahamu kuwa wanahitaji kufanya mabadilko. Na ndio maana wanaenda taratibu sana.
WIMBI LA MABADILIKO
Tangu mabadiriko makubwa ya siasa kutokea huko Tunisia na Misri, walibya nao walihamasika sana mpaka wakaamua kuundoa utawala wake. Walianzia Benghaz na wakaendelea hivyo kuelekea Mizrata na hatimaye Tripoli. Siku za mwisho hapa waliingia Benwalid na Sirte kwenye NGOME ZA MUAMAR GADDAFI. Mapigano huko yalikuwa makali sana na hatimaye NTC wamakuwa wakipata ushindi ingawa kwa kumwaga damu nyingi.
KIFO CHA GADDAFI
Jana tarehe 20 Oktoba 2011 habari zilipatikana kupitia Aljazira kuwa Gaddafi amekamatwa akiwa amejeruhiwa miguuni. Lakini saa moja baadaye habari zikatoka kwa Kanal wa Jeshi mwenye nguvu kuliko wote Africa Muamar Gaddafi ameuawa. Taarifa zinaonyesha alikuwa amejificha kwenye kalvati ndipo askari wa NTC walipomshambulia na kumjeruhi na hatimaye kifo chake.
Shimo au kalavati ambamo Kanali Gadaffi alijificha kabla ya kufa kwake.
Hii ndiyo Bunduki aliyokutwa nayo marehemu Gadaffi
Picha Gadafi baada ya kuuawa