Powered By Blogger

Tuesday, April 12, 2011

Wivu katka mapenzi

 Wanasaikolojia ya Uhusiano na Mapenzi wanaeleza kuwa, wivu katika mapenzi una umuhimu wake lakini pia wanadai kuwa wivu ukizidi huweza kuharibu kama sio kuvunja kabisa uhusinao. Hata katika mitaa tunayoishi naamini kuwa unaweza ukawa umesikia matukio kadha wa kadha yanayosababishwa na wapenzi baada ya kuoneana wivu.

Katika hili kuna ukweli ndani yake, unajua unapopenda kitu lazima ukionee wivu, hutapenda kuona kama kuna mtu anayekuingilia katika kitu chako.
Maana halisi ya mapenzi ya kweli ni yale ambayo hutegemei kuachana na mpenzi wako katika siku zote za maisha yako. Hii humaanisha kuwa ndoto zako juu ya mpenzi wako ni ndoa na sio vinginevyo, sasa kama ukihisi kuna mtu anayekuingilia lazima uwe na wivu.
stock photo : Loving couple embracing
“Siku nikimkuta mpenzi wangu yupo na mwanamke chumbani sijui itakuwaje? Lakini lazima nimkomeshe huyo mwanamke aliyenaye kwanza, siwezi kuibiwa nikiona!” Hayo ni maneno ya dada mmoja anayefanya kazi katika Salon moja ya kiume iliyopo Kariakoo, baada ya kuzungumza nami hivi karibuni.
stock photo : Attractive African American Man, Woman and Child posing in the park.
Katika kauli yake nilijifunza kitu muhimu sana, yaani alimaanisha kuwa hata kama angewakuta wapo katika hali ya kawaida lazima angesababisha mtafaruku kwa kuwa amewakuta chumbani. Hii ni aina mbaya ya wivu, kwa sababu unawza ukasababisha madhara makubwa, lakini baada ya kuwa umeshasababisha madhara hayo ndiyo unaanza kujutia baada ya kusababisha madhara makubwa.

WIVU KIPIMO CHA MAPENZI

Mapenzi ya kweli huanzia kwenye wivu, lazima umwonee mpenzi wako wivu! Kamka una mpenzi wako halafu hakuonei wivu anza kumchungumza vizuri, huenda akawa ahana mapenzi ya kweli kwako japokuwa jambo hili linategemeana. Unapoonyesha unamwonea wivu mpenzi wako, unakuwa unaonyesha thamani ya mapenzi yake kwko.

Yaani unaonyesha ni jinsi gain ambavyo maisha yako hayawezi kukamilika bila yeye, ukimwona yupo katika mazingira ‘tata’ haraka unamhoji ili akupe ukweli. Mpenzi wako atakapopgundua kuwa una wivu naye, ni wazi kuwa ataongeza mapenzi kwako na kama aalikuwa hana ‘time’ na wewe huo utakuwa wakatinwake mzuri wqa kuachia ngazi!
stock photo : A happy couple embraces each other in front of a neutral background in landscape format

Tafiti mbalimbali za wataaalamu wa Uhusiano zinaonyesha kuwa, unapomsingizia au kumzonga sana mpenzi wako kuwa amefanya jambo fulani baya hasa la usaliti, unamweka klatika ushawishi wa kufanya jambo hilo ili kuaendana sawa na tuhuma unazompa.
stock photo : young happy african american couple watching TV on sofa
Siku zote fanya uchunguzi kabla ya kuafanya uamuzi wa jambo lolote kwa mwandani wako. Ninapozungumzia suala la wivu, sina maana kuwa ni wanawake peke yao bali hata wanaume nao huingia katika mkubo huo wa wivu.
stock photo : Young happy couple embracing in an empty house
Mpende sana mpenzi wako, lakini usizidishe wivu juu yake. Onyesha kuwa unampenda na kumjali, onyesha unavyojisikia vibaya ukiibiwa penzi lako lakini kamwe usimtuhumu mwandani wako katika jambo ambalo bado hujalifanyia utafiti wa kutosha.
 
Source: imeazimwa
 
WIVU UNAPOZIDI…
Hapo sasa ndio mwanzo wa matatizo! Ni kweli unampenda mpenzi wako lakini usizidishe wivu kwake. Unapozidisha wivu hata ladha ya mapenzi hupungua, anatambua kuwa unampenda lakini utakapoanza kumchunga sana, inakuwa kero.
“Nishakuzoea kila siku unanijia nyumbani usiku, unatoka kwa wanawake zako huko ndio unakuja kwangu, sawa tu!” Kauli kama hii sio muafaka kwa mwandani wako. Una uhakika gain kuwa mumeo ametokea kwa wanawake? Acha papara, kaa nay echini zungumza naye kwa sauti nzuri, tumia hekima yako naamini atakuambia ukweli amewtoka wapi.

No comments:

Post a Comment