Kutoka vyombo mbalimbali (agathon Kipandula)
***************************
Kutupwa watoto Mwananyamala |
Tuesday, 02 February 2011 |
*Wamama 3 na baba watambuliwa
*Tume yaundwa, kutoa tamko leo
***************************************
MAITI za watoto 10 zimekutwa zikiwa zimefukiwa kwenye shimo moja huku zikiwa zimefunikwa kanga na mashuka ya Hospitali ya Mwananyamala ya jijini Dar es Salaam.
Maiti hizo zimekutwa katika eneo la Mwananyamala Msisiri, jijini Dar es Salaam, pembezoni mwa makaburi ya kwa Kopa mita chache kutoka katika hospitali hiyo.
Akizungumza na Mwananchi jana, Amour Mbaga, anayeishi kwenye eneo hilo, alisema alibaini hali isiyokuwa ya kawaida wakati akifanya usafi jana saa 3.00 asubuhi.
“Wakati nafanya usafi niliona shimo la takataka likiwa limefukiwa mchanga, nikashangaa shimo halikuwa limejaa taka, lakini limefukiwa, nikajiuliza ni nani kafukia, wakati naangalia nikauona mkono wa mtoto,”alisema.
Alisema aliwaita majirani na kuwajulisha polisi wa kituo kidogo Mwananyamala kwa Kopa na baadaye Kituo cha Polisi cha Oysterbay.
*******************************************
MADAKTARI wamepatwa na wakati mgumu baada ya kubanwa walipokuwa wakijichanganya kutoa maelezo ya awali kuhusuwatoto 10 waliokutwa wamezikwa katika shimo moja Mwananyamala kwa Kopa Dar es Salaam.
Tukio hilo lilitokea jana katika Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Bw. Jordan Rugimbana katika mkutano wa waandishi wa habari na madaktari, Mkurugenzi Mtendaji wa Manispaa, Kamanda wa Polisi Kinondoni na watendaji wengine wa wilaya hiyo.
Taarifa iliyotolewa na Bw. Rugimbana ilikuwa ikieleza kuwa watoto watatu walizaliwa wakiwa wafu, watoto saba walizaliwa kabla ya wakati na wote walikabidhiwa kwa wazazi kwa ajili ya maziko.
*******************************************
Viliviringishwa shuka ya Mwananyamala
Kina cha kaburi ni kifuti moja na nusu tu
Tukio la kuogofya la kuzikwa katika kaburi la pamoja kwa vichanga 10 limetokea jijii Dar es Salaam, huku umma ukipigwa butwaa na hali hiyo. Hali hiyo iligundulika jana eneo la Mwananyamala Kwa Kopa, karibu na nyumba ya mkazi mmoja aliyetajwa kwa jina la Mariamu Harubu, jirani na makaburi ya Mwananyamala.
Watoto wote walikutwa wamezikwa kwenye jalala la nyumba ya mkazi huyo, wakiwa wamefukiwa chini kina cha futi moja na nusu. Hali hiyo iliyozua taharuki katika eneo hilo kwa kuvuta kundi kubwa la watu, ilitokea jana mchana, wengi wakiwa hawaamini macho yao miili hiyo ilipochimbuliwa kwenye kaburi hilo.
Mkazi wa jirani na nyumba hiyo ambaye hakutaka jina lake liandikwe gazetini, alisema watoto hao walikutwa wakiwa wamevingirishwa kila mmoja katika kanga yake na kufunikwa kwa shuka moja ************************************************
|
maiti za watoto waliofukiwa Mwananyamala (from
michuzijr.blogspot.com)
MAONI YETU (KWA UFUPI)
Tukio la kukutwa watoto 10 wakiwa wamefukiwa kwenye shimo huko Mwananyamala ni la kushangaza na kusikitisha sana. Inashangaza kwa sababu tukio hili limefanywa Tanzania nchi ambayo tunajulikana kuwa ni ya Amani na Utulivu. Inasikitisha kwa sababu kwa vyovyote vile umehusishwa watu wazima, wenye akili na WASOMI wa hospitali ya Mwananyamala.
Hili jambo linashanga kwa mambo mengi sana:
Watoto kumi wanakutwa shimo moja wakiwa wamefukiwa kwenye shimo la futi moja tu!
Watoto 10 wamepatikanaje mpaka wazikwe shimo moja? Maana siamini kama watoto kumi wanaweza kufa kwa siku moja. Kama hilo linawezekana basi Taifa linatakiwa lifanye uchunguzi upya wa idadi ya watoto wanao zaliwa na wanaokufa kwenye hospitali zetu. Panatakiwa kauli ya Waziri hapa.
Kwamba wazazi wanakabidhi maiti zao chumba cha maiti ili wao wazike ni jambo geni pia. Tumeona mara nyingi kwamba mkifiwa na mtoto kabla ya kutoka hospitali mnapewa wazazi na mnazika hapohapo kwenye makaburi ya karibu na huwa ni siku HIYOHIYO.
Kwamba hospitali ambayo wafanyakazi wake wote wamebadirishwa ndiyo wameshiriki jambo hili inatia shaka kwenye sekta yote ya afya. Inaonyesha kuwa mambo hayo yanafanyika pia sehemu nyingine nchini.
Kwamba kuna Mtanzania mwenye akili timamu anaweza kuzika watoto 10 kwenye shimo moja ni jambo la kushangaza sana. Hapa kwa kweli tunapaswa kupima utu wa watu wote hao ambao wametumika kuzika wato hao.
Tunaiomba serikali ichukue hatua stahili ili wahusika wote wakiwemo WAZAZI, WAUGUZI NA WALIOSHIRIKI KUZIKA MAITI HIZO.
No comments:
Post a Comment