Powered By Blogger

Monday, January 17, 2011

Mapendekezo ya marekebisho ya sheria za mpira wa miguu

MAPENDEKEZO YA SHERIA ZA MPIRA WA MIGUU (I)
Mchezo wa mpira ni mchezo unaopendwa sana na mamilioni ya washabiki kote duniani. Mapenzi haya ya mpira wakati mwingine yanavurugwa na sheria mbalimbali ambazo zimeonekana ni kikwazo kwa maendeleo ya mpira.

Kikwazo hicho kinaweza kuwa kinatokana na udhaifu wa sheria au ni udhaifu wa mwamuzi mwenyewe. Hapa najaribu kutoa mapendekezo machache ili kuona kama yanaweza kuifanya  jamii ya wapenda michezo wa Tanzania na kote ulimwenguni wakapata furaha zaidi kupitia mpira wa miguu.

1.      Golikipa kuuzuia mpira unaotoka kwa adui kwa miguu na kisha kuushika kwa mikono yake.
Mpaka hivi sasa sheria ya mpira wa miguu inamrusu Golikipa kuuzuia mpira uliopigwa na adui yake kwa miguu yake na BAADAYE kuushika mpira huo kwa mikono yaani kuudaka.

Utaratibu huu umekuwa ukitumiwa vibaya na magolikipa kupoteza muda. Mara nyingi Golikipa huutuliza mpira huo kwa miguu na mara adui yake anaposogea karibu golikipa huyo huuchukua mpira huo kwa mikono yake. Hatua hii hupoteza muda mwingi sana hasa kwa timu ambayo imefungwa au inaelekea kupoteza mchezo huo na has zinafika dakika za mwisho za kipindi cha pili cha mchezo.



Mapendekezo:
Golikipa asiruhusiwe kuushika kwa mikono mpira ambao ameutuliza kwa miguu yake. Ikitokea hivyo mpira huo uhesabiwe kama pasi ya nyuma (back pass) hivyo adhabu stahili itumike. Hatua hii inategemewa kuokoa muda unaopotezwa na magolikipa wa timu inayoongoza.

No comments:

Post a Comment