Powered By Blogger

Saturday, January 29, 2011

Polisi na waandamanaji wapambana Misri

Polisi wamepambana na maelfu ya waandamanaji kwenye mji mkuu wa Misri, Cairo, baada ya sala ya Ijumaa wakitaka Rais Hosni Mubarak ajiuzulu.
Polisi walirusha mabomu ya machozi na kutumia mizinga ya maji kusambaza watu, waliokuwa wakirusha mawe.
Watu hao pia waliandamana katika miji ya Suez na Alexandria.
Maandamano Misri

Serikali ilisema iko tayari kwa mjadala, lakini pia imeonya kuchukua "hatua madhubuti".
Mawasiliano ya kupata huduma za wavuti na simu za mkononi yamekatizwa.

No comments:

Post a Comment