Powered By Blogger

Saturday, January 29, 2011

Mpenzi wa jinsia moja auawa Uganda

David Kato

David Kato
Mwanaharakati wa kutetea haki za wapenzi wa jinsia moja wa Uganda ambaye mwaka jana alilishtaki gazeti lililomtoa kwa jinsia yake hiyo amepigwa mpaka kufa.

Polisi wamethibitisha kifo cha David Kato na kusema wamemkamata mshukiwa mmoja.
Gazeti la Uganda la Rolling Stone lilichapisha picha za watu kadhaa ambao walisema ni wapenzi wa jinsia moja na huku pembeni kukiwa na kichwa cha habari "Wanyonge"

Mapenzi ya jinsia moja ni kinyume na sheria Uganda, na adhabu ya miaka 14 jela.

No comments:

Post a Comment