Powered By Blogger

Wednesday, November 3, 2010

KUTAMBULISHA BLOG

Katika Blog hii nitakuwa nawaletea makala mbalimbali za kuhusu, ndoa, uhusiano na michezo. Mambo mengi ya michezo kimataifa yanajulikana lakini kinachotakiwa ni kuwekwa mahali pamoja ambapo wadau wanaweza kuyapata kwa urahisi zaidi.

Mambo mengine ya mahusiano na ndoa ni ya siku nyingi sana lakini maisha ya ndoa yamekuwa yakibadirika sana kuendana na mabadiriko na mfumo wa maisha. Katika makala hizi za ndoa na mahusiano nitawaletea makala mbalimbali kutoka wa wahadhiri wakubwa duniani kama Nancy VanPelt na wengine wengi.

Makala hizi zitakuwa zinaletwa kwenu kila nafasi inapopatikana ingawa lengo langu ni kuzileta kwenu kila siku.

Sababu ya kuwaletea makala za ndoa na mahusiano
1. Maisha ya kisasa kimsingi yamekosa usimamizi wa kifamilia hasa kuhusu ndoa na mahusiano. Kwa wale ambao wamezaliwa siku za nyuma watakumbuka kuwa kulikuwa na jando na unyago kwa vijana wa kike na wa kiume. Kwa sasa ukiondoa baadhi ya makabila kama (Watani zangu Wazaramo, Wakwele na Chinga family) wengine tunaishi maisha ya Ki-Tanzania ambayo mila yetu ni Kiswahili tu. Kutokana na hilo vijana na baadhi ya wakubwa ambao hawakubahatika kupata elimu hii watafaidika na mafundisho haya.

2. Mahusiano ya ndoa na mapenzi ni elimu kama zilivyo elimu nyingine duniani hivyo zinahitaji kufundishwa. Ni wazi kuwa kama hujapata mafundisho ya ndoa, mahusiano na mapenzi utakuwa una mapungufu katika mahusiano na mwenza au wenza wako hivyo kushindwa kutimiza baadhi ya majukumu yako "kindoa".

3. Uzoefu unaonyesha kuwa kuna nyakati mbalimbali aidha mwenza wako au wewe mwenyewe umefundishwa jinsi ya kufanya jambo au mtindo fulani katika mapenzi au mahusiano ambao hukuwahi kuona kabla. Hiyo inakuonyesha wazi kuwa hakuna mtu anaweza kujua kila kitu bila kufundishwa na wengine.

4. Maisha ya kisasa yamejaa changamoto nyingi za maisha, malezi na mahusiano na zote hizi zinapaswa kueleweka rasmi theoretically.

Naamini makala hizi mtazipenda na kuzifurahia sana maana wengi wenu hasa nyie wa dot.com mtapata mengi ingawa hata wakongwe mnaweza kuambulia baadhi ya mafunzo.

Kila la heri.

No comments:

Post a Comment