Mgombea wa Chama Cha Mapinduzi Dr. Jakaya Mrisho Kikwete aak Mkwele ameshinda kinyang'anyilo cha uchaguzi wa Urais Tanzania kwa kupata kura nyingi kiasi cha asilimia 61. Wanaomfuatia Dr. Slaa wa CHADEMA amepata asilimia 26 na Prof Lipumba amepata asilimia 8.
Taarifa kamili kama inavyoonyeshwa hapa chini:
- Watu waliojiandikisha kupiga kura walikuwa 20,137,303 (idadi hiyo ilipungua hadi Milioni 19 kutokana na sababu mbalimbali zikiwemo za vifo, safari, kupoteza shahada, nk).
- Watu waliopiga kura walikuwa 8,626,283 sawa na asilimia 42.84% (ya wote waliojiandikisha)
- Kura zilizoharibika ni 227,889 ambazo ni asilimia 2.64% ya kura zote zilizopigwa.
- Kura halali zilikuwa 8,393,394 yaani asilimia 97.36% ya kura zote zilizopigwa.
Matokeo kwa mlinganyo wa kura kwa vyama na wagombezi wake ni kama ifuatavyo:
- Dovutwa Yahmi Nassoro/UPDP kura 13,176 = 0.15%
- Mgahywa Muttamwega Bhatt/TLP kura 17,482 = 0.20%
- Rungwe Hashim Spunga/NCCR-Mageuzi kura 26,388 = 0.31%
- Kuga Peter Mziray/APPT Maendeleo kura 96,933 = 1.12%
- Lipumba Ibrahim Haruna/CUF kura 695,667 = 8.06%
- Slaa Willibrod Peter/CHADEMA kura 2,271,941 = 26.34%
- Kikwete Jakaya Mrisho/CCM kura 5,276,827= 61.17%
Tunampongeza Ndugu Kikwete, wagombea wote wa urais na wengine wote walioshiriki katika uchaguzi huu ambao ulikuwa wa ushindani mkubwa sana kwa mara ya kwanza tangu mwaka 1995.
Mungu Ibariki Tanzania
No comments:
Post a Comment