Powered By Blogger

Monday, December 6, 2010

MKENYA MWENYE WAKE 120 AZIKWA

Mwanaume wa nchini Kenya aliyejulikana kwa jina la Ancentus Akuku maarufu kwa jina la " Akuku Danger" ambaye huenda akawa mwanaume aliyeoa wanawake wengi kuliko wanaume wote duniani, ambaye alifariki dunia akiwa na umri wa miaka 94 amezikwa jana jumapili 5 Desemba 2010


Katika maisha yake, Akuku alioa jumla ya wanawake 130 kati ya wake zake hao 30 aliwapa talaka.

Kama jina lake linavyobashiri "Danger", (hatari), Akuku alikuwa na watoto 210, wakiume 106 na wakike 104. Kati yao watoto wake wa kike 35 na wa kiume 20 wamefariki dunia.


Kwa mujibu wa mtoto wake mkubwa, Akuku alizimia akiwa kwenye mazingira ya nyumba yake mjini Kisumu, alipowahishwa hospitali alifariki dunia.

Akuku alimuoa mke wake wa kwanza Dinah Akuku, mwaka 1939, wakati mwaka 1997 akiwa na umri wa miaka 79, Akuku alifunga ndoa na msichana kigori mwenye umri wa miaka 18. Huyo ndiyo alikuwa mwanamke wa mwisho kufunga ndoa na Akuku.

Mazishi ya Akuku aliyefariki jumamosi yamekumbwa na mzozo kutokana na idadi kubwa ya watoto. Hadi sasa muafaka haujafikiwa kuhusiana na tarehe ya kuzikwa kwake.

Ukoo wa Akuku una shule mbili zilizojengwa na Akuku ili kuwapa elimu watoto na wajukuu zake na pia wanamiliki kanisa lao moja kwaajili ya ibada.


Dr Tom Akuku ambaye ni mtoto mkubwa kuliko wote wa kiume wa Akuku, alisema kuwa ingawa hati walizo nazo zinaonyesha Akuku ana watoto 210, huenda baba yao akawa na watoto zaidi ya 210.

"Mzee alikuwa na watoto wa kike 104 na wa kiume 106 hivyo kufanya jumla ya watoto 210, lakini naamini kutakuwa na watoto wengi hawamo kwenye listi".

"Idadi ya wajukuu ni zaidi ya 1,800", alimalizia kusema Dr. Akuku.

5 comments:

  1. jamaa alikua na nguvu zaid ya simba lakini pia alikua na akili nyingi kwasababu asingejenga shule watoto wake wangepata tabu

    ReplyDelete
  2. hahahahahah this is sweet! he lived his life to the fullest!!

    ReplyDelete
  3. This comment has been removed by the author.

    ReplyDelete
  4. Dear Kipandula
    Hello.
    I'm Fumito Takahashi,working in Yomiuri Television(Osaka,Japan).
    I want to introduce your picture in our program.
    That picture is posted in "MKENYA MWENYE WAKE 120 AZIKWA
    "(In Dec 2010).
    Can I broadcast your picture?
    I'm waiting for your reply.

    Fumito Takahashi
    e-mail: fumito.takahashi@ytv.co.jp

    ReplyDelete