Utamaliza mabucha nyama ni ile ile ni mzemo mashuhuri sana katika jamii na mara nyingi hutolewa na ile jinsi pinzani ambayo kwa siku za karibu imepanda chati sana hapa Tanzania.
Kwa maoni yangu msemo huu umekaa katika hali ya kiuvivu sana. Kimantiki, katika hali ya bucha za kawaida nyama hutofautiana kutegemea na aina ya nyama (hapa tunaongelea nyama ya ng’ombe tu). Kuna nyama ya ng’ombe wa Maziwa na wale wa nyama na radha ya nyama hizi hutofautiana sana.
Lakini pia kuna nyama ya ng’ombe wa kienyeji wanaotoka Usukumani au Ukuryani na wale wanaotoka kwenye Ranchi hasa pale Kongwa. Ni wazi kuwa nyama ya Ngombe wa Kongwa na Shinyanga ni tofauti na sababu ziko nyingi na wazi. Matunzo, mazingira, na kubwa zaidi ni Maumbile! Kama vile ambavyo nyama hiyo inatofautiana ndiyo bucha zake zitakavyovutia watu tofauti kutokana na sababu za hapo juu.
Kwa upande wa zile Bucha zile nyingine (kwani nazo ni bucha kweli? Teh teh teh )hali ni hivyo hivyo, matunzo, mazingira na Maumbile ni vitu muhimu sana. Nawaasa wauzaji wake waache uvivu, warekebishe matunzo, mazingira na mambo yatakuwa sawa. Tusirahishe mambo sisi walaji tunaona tofauti kati ya nyama ya bucha moja na nyingine kutogemeana na kama inatoka Maswa au Kongwa!.
Just for the sake of it...
Just for funny
No comments:
Post a Comment