Powered By Blogger

Friday, December 10, 2010

Bwanaharusi, wakwe washikiliwa na polisi Tanga

BWANAHARUSI ambaye ni mkazi wa Kijiji cha Mandela Kata ya Segera wilayani Handeni mkoani Tanga pamoja na wakwe zake wawili, wanashikiliwa na polisi kwa tuhuma ya kuoa mwanafunzi wa darasa la tano katika Shule ya Msingi Kwedizinga Kata ya Kwedizinga.

Nadhani watakuwa wanafanana na hawa!


Wazazi wawili wa binti huyo, wanashikiliwa kwa tuhuma ya kumkatiza masomo binti huyo mwenye umri wa miaka 14 na kumuoaza kwa mwanaume huyo ambaye jina lake tumelihifadhi.

Ofisa Mtendaji wa Kata ya Kedikwazu Rukia Kizinga, alisema ndoa hiyo, ilifungwa juzi wilayani Handeni.

Kizinga alisema baada ya kumaliza kufunga ndoa, walipanda kwenye magari na kuanza msafara wa kuelekea Mandera, lakini polisi wa kituo cha Kabuku waliwakamata.

"Ni kweli hapa kuna binti wa darasa la tano mkazi wa kitongoji cha Ugweno,amefungishwa ndoa na mwanaume mmoja wa Kijiji cha Mandera. Wakati ndoa hiyo ikifungwa, polisi walikuwa wakiandaa mazingira ya kuwanasa.

“Baada ya kufunga ndoa na maharusi kuanza kuondoka, walinaswa katika eneo la stendi,” alisema.


Kizinga alisema watu wote wanashikiliwa na polisi na kwamba walikuwa wakiangaika kupata dhamana," alisema Ofisa Mtendaji huyo.

Baadhi ya mashuhuda wa tukio hilo, walionyesha kushangazwa na familia hizo mbili kufanya tukio la kufungisha ndoa vijana hao huku wakitambua binti huyo ni mwanafunzi.

"Hawa watu inaonyesha ni jinsi gani hawaogopi ama kupuuza mamlaka zinazowatawala. Hivi unaamini kwamba hawajui kwamba kumuoza au kuoa mwanafunzi tena wa Shule ya msingi ni kosa?," walihoji watu hao.

source: Mwananchi newspaper

No comments:

Post a Comment