Powered By Blogger

Friday, December 31, 2010

MADHARA YA POMBE KWENYE NDOA NA MAHUSIANO

Ndoa nyingi siku hizi hasa zile za Kikristo huanza na pombe (champagne au pombe nyinginezo) ingawa usasa nao umefanya madhehebu mengine nayo yatumie pombe kwenye sherehe zao. Katika hali ya kawaida kabisa maharusi katika siku yao ya kwanza kuwa pamoja wanakuwa wamelewa! Wengine hulewa sana kiasi cha kusahau hata wajibu wao wa NDOA angalau kwa siku hiyo muhimu!
 
Pombe ni moja ya chanzo cha matatizo makubwa sana katika ndoa nyingi ingawa wanandoa wanaokunywa huwa hawapendi sana kuzungumzia tatizo hili sugu. Tatizo hilo ni kubwa sana ingawa kwa Wamarekani nusu ya Wanandoa wa Marekani ni walevi ! Hii haijalishi kama mlevi ni bwana au bibi harusi wa ndoa hiyo. (Hapa sizungumzii wanywaji bali nazungumzia WALEVI)
 
Pombea imekuwa na madhara makubwa sana kwenye mahusianao ya wanandoa wengi kiasi cha kuathiri ndoa hizo. Baadhi ya madhara hayo ni:
  1. Vurugu katika ndoa ni mambo yanayotarajiwa katika familia ya wanandoa walevi. Ugomvi wa mara kwa mara ni mambo ambayo yameripotiwa kwenye ndoa nyingi sana kote duniani.
  2. Pombe inasababisha kuvunjika kwa mawasiliano miongoni mwa wanandoa. Mawasiliano kwa wanandoa ni moja ya matatizo makubwa sana kwenye ndoa. Makala maalum kuhusu mawasiliano italetwa kwenu siku zijazo.
  3. Hasira ni moja ya matatizo yanayoletwa na pombe kwenye ndoa. Mwanandoa ambaye tabia yake ni ya kawaida lakini baadhi wakinywa pombe wanabadilika na kuwa hasira nyingi na hilo linakuwa ni tatizo katika mahusiano yao.
  4. Ulevi na pombe vinaweza kusababisha kutowajibika katika ndoa. Pombe inaweza kuwa inakula bajeti yote ya matumizi ya nyumbani kiasi cha kukosa kabisa fedha za kutunza familia.
  5. Ulevi huleta matatizo ya kisaikolojia kwa mwanandoa asiyekunywa. Matatizo hayo ya kisaikolojia yakichanganyika na matatizo ya huyo mwenzake mlevi basi ndoa hiyo itawaka moto.
  6. Pombe ni chanzo kikubwa sana cha taraka na kuvunjika kwa ndoa. Mkusanyiko wa matatizo yote yaliyotajwa hapo juu yanachochea sana kuvunjika kwa ndoa.
  7. Ulevi humfanya mwanandoa kujihusisha sana na wapenzi wengi sana (multiple sexing). Hili ni tatizo sugu siku hizi maana uwepo wa magonjwa kama UKIMWI inakuwa ni kikwazo sana kwa maendeleo ya ndoa.
  8. Katika baadhi ya ndoa matatizo ya ulevi yamehusishwa na “unyumba!” Fakiria baba mlevi, mama mlevi wote wanalewa kila siku wanarudi hoi kiasi cha kukosekana yale mambo yetu! Hapo tena panaweza kuzalewa tatizo jingi la kukosa watoto maana watoto wanapatikana tu baada ya kupitia hatua hizo.
  9. Baadhi ya wanafamilia wamelipoti pia matatizo ya nguvu za kiume baada ya kulewa pombe. Hapa tena tatizo linakuwa kubwa zaidi maana ndoa yenyewe ndiyo inaelekea kufa na siyo kuvunjika.
 
Kwa ujumla matatizo yaletwayo na pombe na ulevi kwenye ndoa ni mengi sana. Wanywaji wengi husema watu wasiokunywa pombe wanamatatizo yao kwenye ndoa lakini hili mimi naliona kama sababu tu za kuhalalisha ulevi wao. Hatusemi watu waache pombe ila JAMBO LA MSINGI NI KUWA WATU WAACHE ULEVI.
HERI YA MWAKA MPYA 2011

No comments:

Post a Comment