Powered By Blogger

Friday, November 26, 2010

SIFA ZA KIJINGA (ZA WANAUME)

Najua nitapingwa ila kuna ukweli wapwaaz!

Mara nyingi mazungumzo ya wanaume ni kujisifu kwa Ngono na Ulevi. Unaweza kaa kijiweni na washikaji utasikia oooh mimi nimelala karibu na wanawake wote wa ofisini kwetu na hata mtaani nimechapa sana (anasema haya huku akijua ni uwongo kabisa). Ama mwingine atadakia nimelala jana tu na Khadija na sasa nina miadi na Roselyn (ukifatilia ni uwongo). Hili ni kundi la watu wenye kipato kidogo yaaani wa uswazi.

 

Ukienda kwa wale wasomi nao ni hivyo nilienda seminar na Ms Rebecca Kule Johannesburg, kwa kweli tulikuwa chumba kimoja ili kusave ila tumerudi hapa bongo tunakaushiana. Mwingine naye atakupa issue Mke wa Fidel ni mtamu sana lile ta.ko acha tu nilikuwa naye Ngurdoto kwenye seminar elekezi si pole pole huu ni uwongo pia. Msomi Mwingine utasikia nina Mademu wawili nimewapata JF week end hii nauwa mmojawapo lol


Wengine utasikia mimi kwa pombe ni balaa jana nimekunywa crate la konyagi na konyagi za kopo. Mwingine atachangia acha hizo mimi jana nimepata za kutosha hadi nikafunga bar. Huyu hawa jamaa ukienda nao bar ya ukweli ni beer mbili anaangusha gari ukimuuliza utasikia oooh jana niliwaka sana

Hivi wazee uanaume ni lazima Ngono na Ulevi

No comments:

Post a Comment