Powered By Blogger

Saturday, November 20, 2010

UHUSIANO WA UVUTAJI SIGARA AKINA MAMA NA UHALIFU KWA WATOTO

Utafiti mpya kutoka Marekani unasema huenda watoto waliozaliwa na wakina mama wanaovuta sigara kwa wingi wakati wa uja uzito, wana nafasi kubwa ya kuwa wahalifu wanapo kuwa wakubwa.
Utafiti huo umefanywa na wataalamu wa afya ya umma kutoka chuo kikuu cha Havard, na kutazama watu waliozaliwa miaka ya mwisho ya 1950 na mapema miaka ya 1960.
Sigara
Uvutaji Sigara ni hatari wakati wa uja uzito

Ni wazi, kwa miaka mingi sasa, kuwa uvutaji sigara wakati wa uja uzito kunaweza kuathiri kwa kiasi kikubwa mtoto aliyeko tumboni. Lakini kile ambacho kilikuwa HAKIJATHIBITISHWA, ni kuwa mtoto atakayezaliwa huenda akakua na kuishi maisha ya uhalifu.
Utafiti huo ulitazama maisha ya watu elfu tatu na mia nane waliozaliwa kati ya mwaka 1959 na 1966.

 

Theluthi mbiliKaribu theluthi mbili ya mama zao walikuwa wavutaji sigara wakati wana uja uzito wao, katika miaka hiyo ambayo uvutaji sigara ulikuwa ukikubalika kijamii.
Sigara
Uvutaji sigara

Watafiti hao walipata ruhusa ya kuona taarifa za uhalifu za watu waliokuwa wakiwafanyia uchunguzi.
Watafiti hao wanasema ugunduzi wao umeonesha kuwa watoto wa kina mama wanaovuta sigara nyingi-- yaani wanaovuta zaidi ya sigara ishirini kwa siku -- walikuwa na uwezekano wa asilimia thelathini na moja kukamatwa na vyombo vya dola, kuliko watoto waliozaliwa na kina mama ambao hawakuwa wakivuta sigara kabisa.

Na watoto hao waliozaliwa na kina mama wavutaji, walikuwa na uwezekano mubwa wa kurudia kufanya uhalifu tena, baada ya kukamatwa.

Dokta Angela Paradis, aliyeongoza utafiti huo amesema hajui kwa nini uvutaji sigara wakati wa uja uzito unakuwa na athari ya aina hiyo, lakini utafiti mwingine pia unapendekeza vivyo hivyo.
"Kuna utafiti ambao unaonesha au kupendekeza kuonesha kuwa matatizo hayo yanatokana na athari za kibaiolojia zinazotokana na nicotine katika ubongo unaopevuka, na hilo linaweza kusababisha ugumu katika tabia ya neuro kwa watoto, ikiwa ni pamoja na kutokuwa na umakini na mihemko ya haraka." amesema Dk Paradis.

Familia duni

Wanawake ambao wanavuta sigara wakati wana uja uzito mara nyingi huwa ni wadogo kiumri, na pia hawana elimu ya kutosha na wanatoka katika familia duni, kuliko wanawake wasiovuta sigara wakati wa uja uzito.
Lakini watafiti pia wanasema utafiti wao ulizingatia masuala hayo, na matokeo yalisalia kuwa yale yale. Pia hakukuwa na tofauti kati ya watoto wa kiume na wa kike waliozaliwa kutoka kwa kina mama hao.

Utafiti iliofanywa zamani ulionesha uhusiano mkubwa kati ya uvutaji sigara wakati wa uja uzito na matatizo kadhaa ya watoto, ikiwa ni pamoja na watoto kuwa na nguvu mno, ujeuri, na uhalifu.

No comments:

Post a Comment